Duration 55:51

MALANGO YA NDOTO YANAVYOTUMIKA NA ADUI (V) - PASTOR SUNBELLA KYANDO

17 190 watched
0
222
Published 29 Jul 2021

Kuna ndoto na kuna maono ya usiku.Hivi ni vitu viwili tofauti japokuwa vinawiana sana. Ndoto nyingi zinakuwa na mafumbo,ni ngumu sana kupata ujumbe wa moja kwa moja hadi upate tafsiri ya ndoto hiyo.Maono ya usiku huwa yanakuja na ujumbe wa moja kwa moja.Ni kitu ambacho kwa wakati huo ndio kilikuwa kinaendelea katika ulimwengu wa roho na roho yako imepata uwezo wa kuona.Chochote kinachokuwa halisi sana kwako na kikakuonesha maana kamili ya ulichokiona sio ndoto,ni maono.Maono huwa ni halisi sana,kwa mfano unaweza kuota unakimbizwa,na ukishtuka usingizini unajikuta unahema kwa nguvu,hiyo haikuwa ndoto bali maono. Ukisoma kitabu cha Mathayo; Mathayo 2:13 [13]Na hao walipokwisha kwenda zao, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto, akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuambie; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize. Kama Yusufu angeipuuzia hii ndoto basi maisha ya mtoto yangekuwa hatarini.Lakini pia shetani hutumia ndoto na maono kupitisha vya kwake.Mfano wa hiki kitu tunakiona kwenye kitabu cha Zekaria; Zekaria 10:2 [2]Kwa maana vinyago vimenena maneno ya ubatili, nao waaguzi wameona uongo; nao wameleta habari za ndoto za uongo, wafariji bure; kwa sababu hiyo waenda zao kama kondoo, wateswa, kwa sababu hapana mchungaji. Kuona ndoto wameona lakini za uongo,kama za uongo tayari aliyezileta anajulikana(shetani).Na ndoto inapokuja na ukaipokea ile roho iliyo nyuma ya ile ndoto pia huja ndani yako.Kama ni ndoto kutoka upande wa shetani iwe umeota wewe au umeotwa na ukafungua moyo kuipokea basi na ile roho ya giza itakuja ndani yako.Na ndio maana unatakiwa uwe makini sana na ndoto unazoota au unazootwa.Kabla hujazipokea muulize kwanza Mungu kama ni ya kwake,na kama si yake usiipokee. Katika ibada ya leo tumeendelea kujifunza kwa undani kuhusu namna adui anavyotumia ndoto na maono kupitisha uharibifu.Tunamshukuru Mungu maana amefunua fahamu zetu kwa kiasi kikubwa juu ya lango la ndoto. UNAWEZA WASILIANA NASI AU KUTUMA SADAKA YAKO KWA NAMBA HII : 0657 173 322 Unaweza kutufuatilia katika mitandao yetu ya kijamii Like our Facebook: https://www.facebook.com/Therealityof ... Follow our Instagram: https://www.instagram.com/realityofch ... Subscribe our YouTube: /channel/UC67L ... Also Subscribe Roc worshippers youtube channel:/channel/UCyVhAzjcFaJH7lxgiMQviGQ

Category

Show more

Comments - 17